Ijumaa, 22 Machi 2013

HAIFAHAMIKI KWA

MARTIN KADINDA KUWACHAMBUA DADA WA WEMA SEPETU

 
Na: Mwandishi wetu
Huenda umekuwa ukimsoma tu msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Isack Sepetu bila kujua kuwa ana dada zake ambao wamesimama kimaisha licha ya kwamba si watu wa kuonekana kwenye vyombo vya habari mara kwa mara.
Juzikati, mwanamitindo maarufu wa kiume Bongo, Martin Kadinda kupitia blog yake ya mvutokwanza amewachambua dada watatu wa Wema huku akianika tabia zao kwa jinsi yeye anavyowafahamu kama anavyowaelezea hapa chini;
TUNU: Napenda kumuita The Perfectionalist. Huyu ni mama wa mtoto mmoja, anaishi nchini Marekani. Ni mpole na anapenda kusikiliza watu. Anapenda kuchukua muda kabla ya kutoa maamuzi ya jambo analopenda. Ni mtafutaji na amekuwa akiniita baby.
SUNNA: Huyu ana visirani kama mdogo wake Wema. Anaishi Marekani. Nampenda sana, ni mcheshi na napenda kumuita majimaji kwani anapenda sana kula…yeye ni bata ndefu kwa kwenda mbele.
Ni mpenzi wa fasheni na vitu asilia.
NURU: Ni mama wa watoto watatu, ameolewa na anaishi Dar. Napenda kumuita kubwa la maadui kwani hakuna kinachoshindikana kwake.
Tatizo lolote litakalotokea katika familia yake akionekana tu kila kitu kinakwenda sawa.
Ana ubavu wa kukontroo mambo

Ijumaa, 15 Machi 2013

HAYA KWELI NI YA AIBU

UWOYA, NDIKU USO KWA USO RWANDA

Na Mwandishi Wetu
ZIARA ya mastaa wanne wa Bongo Movies nchini Rwanda hivi karibuni, imewakutanisha uso kwa uso wanandoa waliotengana, Irene Pancaras Uwoya na msakata kabumbu, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ Ijumaa limebaini.
Irene Pancaras Uwoya akiwa na mumewe Hamad Ndikumana ‘Kataut’ enzi za penzi lao.
Uwoya na Kataut walikutana jijini Kigali baada ya mastaa hao kupata mwaliko wa kiserikali kuhudhuria tuzo za filamu zilizoandaliwa kwa ajili ya wasanii wa Kinyarwanda (Rwanda Movies  Awards).
Chanzo chetu kimesema kwamba, wawili hao ambao walifunga ndoa mwaka 2009 jijini Dar na kubahatika kupata mtoto mmoja aitwaye Dagrei Krish, waliongea kwa muda mrefu na kutoonesha tofauti yoyote.
“Hawakuonesha tofauti yoyote, waliongea vizuri, walikula pamoja na kulala hoteli moja,” kimesema chanzo hicho.
Ndoa ya Uwoya na Kataut ilivunjika  mwanzoni mwa mwaka jana kisha ‘shemeji’ yetu huyo kuondoka Dar kurudi Rwanda kuendesha maisha yake ya kusakata kabumbu katika Klabu ya Rayon.
Hata hivyo, Ndikumana amekuwa akikanusha kuvunjika kwa ndoa hiyo kwa kusema kwamba hakuna kati yake na Uwoya aliyekiri hadharani kwamba ndoa yao imevunjika.
Mastaa wengine walioambatana na Uwoya nchini Rwanda ni pamoja na Vincent Kigosi ‘Ray’, Jacob Steven ‘JB’ na Amri Athuman ‘King Majuto’ ambao wote pamoja na Uwoya walirudi nchini Jumanne iliyopita.

KUNA KUSOMA KWELI..?

DENTI WA CHUO AUMBUKA BBM

Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
DENTI wa chuo kimoja kilichopo jijini Mwanza (jina tunalihifadhi) aliyefahamika kwa jina la Fatma Omar amejikuta akiumbuka kwenye mtandao wa BBM baada ya picha zake chafu alizokuwa ‘akimfoadia’ mpenzi wake kuvuja.
Fatma Omar.
Picha hizo zikiwemo zinazomuonesha mwanadada huyo mwenye asili ya Kiarabu akiwa amevaa nguo ya ndani tu zinapatikana mtandaoni na inadaiwa kuwa mwenyewe amejikuta akiugua ghafla baada ya kubaini ameaibika.
Baada ya Ijumaa kuzinasa picha hizo na kubahatika kupata namba zake, mwandishi wetu alimpigia simu Fatma ili kujua kilicho nyuma ya pazia ya picha hizo ambapo alifunguka:
“Jamani hizo picha anayezisambaza ni mwanaume aliyekuwa mpenzi wangu anayeishi Arusha, anaitwa Amin Lema. Siku moja usiku aliniomba nimtumie nikafanya hivyo nikiamini hawezi kunifanyia mchezo mbaya.
“Juzi akaniomba nimtumie pesa kama ambavyo ilikuwa desturi yake, nikamnyima na ndipo uhusiano wetu ukavunjika. Baadaye nikasikia picha zangu za utupu zimevuja, kwa kweli sikuwa na jinsi na nilijua zitafika kwenu ‘so’ fanyeni mnavyoweza,” alisema Fatma.
Jitihada za kumpata Amini hazikuweza kuzaa matunda mpaka tunakwenda mtamboni.

HUKU NAPO SIPO

WAZIRI ACHARUKIA SKENDO YA JACK CHUZ KUJIUZA

Stori: Gladness Mallya na  Hamida Hassan
BAADA ya hivi karibuni msanii wa filamu, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kunaswa akipelekwa kuuzwa kwa mwanaume, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla anadaiwa kuicharukia skendo hiyo ambapo juzikati alimvaa Rais wa Shirikisho la Filamu (TAFF), Simon Mwakifwamba na kumuuliza juu ya tukio hilo la aibu.
Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya shirikisho hilo kililitonya Ijumaa kuwa, Mhe. Makalla alimvaa Mwakifwamba kwenye mkutano na wasanii uliofanyika ndani ya Hoteli ya Kibadamu, Ubungo jijini Dar.
“Mhe. Makalla ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, akiwa pale alimuuliza Mwakifwamba kuhusu hatua walizochukua kwa Jack Chuzi baada ya kuandikwa habari kuwa alinaswa akienda kuuzwa.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla.
“Mwakifwamba alijitetea kuwa, wanalishugulikia na Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Michael Sangu ‘Mike’ akasisitiza kuwa, wako katika mchakato wa kulitolea uamuzi tukio hilo lililofanywa na Jack ,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi paparazi wetu alimtafuta Mwakifwamba lakini hakuweza kupatikana mara moja ila Mike alipoulizwa juu taarifa za Mhe. Makalla kucharukia ishu ya Jack alisema:
Rais wa Shirikisho la Filamu (TAFF), Simon Mwakifwamba.
“Ni kweli waziri aliuliza kuhusu hatua tulizozichukua kuhusu suala la Jack kujiuza ambapo nilimjibu kuwa tuko kwenye mchakato wa kulitolea uamuzi na kwa sasa tumeunda kamati maalum, ikimaliza uchunguzi wake ndiyo tutatoa jibu kuwa tumemchukulia hatua gani.”

KWENYE

‘BIRTHDAY’ YA MTOTO WA SAJUKI,MAJONZI MATUPU

Na Imelda Mtema
‘BIRTHDAY’ ya mtoto wa aliyekuwa msanii wa filamu Bongo, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ na mjane wake, Wastara Juma, Farheen ilikuwa ni simanzi tupu, Ijumaa lina fulu data.
Katika pati hiyo iliyofanyika nyumbani anapoishi Wastara, Tabata-Bima, Dar hivi karibuni wakati mtoto huyo akitimiza mwaka mmoja, pamoja na kukamilika katika kila idara lakini kukosekana kwa baba wa mtoto (Sajuki), ndiko kulikoibua huzuni.
Habari zilieleza kuwa Sajuki alikuwa mtu muhimu kwenye pati hiyo kwani siku zote alikuwa akiisubiri siku hiyo ya kuzaliwa mtoto wake kipenzi kabla ya kukutwa na umauti Januari 2, mwaka huu.
Huku kila kona nyumbani hapo kukitawaliwa na huzuni kwa wahudhuriaji, mtoto huyo aliwaondoa watu kwenye simanzi baada ya kuonesha uchangamfu wa ajabu hadi kusababisha mama yake na wageni wengine waalikwa kuchangamka vilivyo kama vile alikuwa anatimiza zaidi ya umri wa mwaka mmoja.
Katika hali ya kushangaza, pamoja na kutulizwa lakini Farheen aliendelea kung’ang’ania kufanya kila kitu mwenyewe hasa lilipofika suala la ukataji wa keki.
Katika mahojiano na Ijumaa juu ya tukio hilo, Wastara alisema kuwa alifarijika mno kumwona mwanaye akiwa na furaha tena mchangamfu kupita kiasi kwani alimfanya asahau machungu.

HILI HATULIFUMBII MACHO..

NANI ALIYEMTOBOA JICHO ABSALOM KIBANDA?

Na Mwandishi Wetu
SHAUKU ya kila Mtanzania ni kumjua nani au ni akina nani waliohusika katika kutekeleza tukio baya la kumshambulia hadi kumtoboa jicho Mhariri Mkuu wa New Habari Corporation, Absalom Kibanda.
 Absalom Kibanda akiwa na mkewe, Anjella Semaya, ndani ya ndege wakielekea nchini Afrika Kusini jana jioni.
Kibanda alikumbwa na tukio hilo usiku wa Februari 5, mwaka huu nje ya nyumba yake, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kibanda mwenyewe, awali alikuwa Sinza akiangalia mechi kati ya Real Madirid na Manchester United ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na baada ya hapo alirejea nyumbani kwake akiwa ndani ya gari lake.
Alisema alipofika nje ya geti kabla hajafunguliwa, walitokea watu asiowajua na kumshambulia hadi kumuachia majeraha sanjari na kumtoboa jicho la kushoto.
Mengi yameshasemwa kuhusu tukio hilo ambapo wengine wanasema waliolitekeleza ni majambazi, wapo wanaodai ni mambo binafsi lakini baadhi wana wasiwasi na mambo ya kisiasa.
Absalom Kibanda akiwa ICU.
MAJAMBAZI
Ni vigumu kuwaingiza majambazi au vibaka katika tukio hilo kwani akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili alikolazwa kwa matibabu, Kibanda mwenyewe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri alisema baada ya watu hao kumaliza kusudio lao hawakuondoka na kitu. Siku zote inajulikana, jambazi au kibaka huvamia mtu kwa kulenga kuondoka na kitu.
MAMBO BINAFSI
Watu wanaodai tukio hilo ni la mambo binafsi wanaweza kuwa na hoja, kwani ukweli wa madai hayo unaweza kuwa ndani ya nafsi ya Kibanda mwenyewe kwa vile ndiye anayejua anaishije na watu. Lakini kwa mujibu wa Kibanda mwenyewe, watu hao wakiwa wanamshambulia hakuna aliyekuwa akizungumzia lawama ya kisasi chochote cha  maisha yake ya kila siku.
Baadhi ya majeraha aliyoyapata Kibanda.
MAMBO YA KISIASA
Hapa ndipo penye sauti nyingi za wadau. Wengi wanasema siasa, hasahasa mchakato wa urais 2015 ndiyo umekuwa ukitajwa sana.
Mtu mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema:
“Unajua Kibanda aliwahi kuwa mhariri wa upande mwingine, akaondoka na sasa yupo kwa Bashe wa CCM. Inawezekana kuna watu wametumia nafasi hiyo, wameona kama amesaliti,” alisema mtu huyo.
Hata hivyo, mtu huyo alisema kuwa  pia Kibanda anaweza kuwa ameteswa na kambi za urais ndani ya chama kimoja cha siasa.
“Uchaguzi ni 2015, kwa vyovyote vile yeye kama mhariri atakuwa ana kambi yake, kwa hiyo kuna uwezekano ameshawahi kuandika habari iliyoathiri kambi nyingine, hilo nalo linawezekana. Lakini katika yote, tukio lake si la binafsi wala ujambazi,” alimalizia mtu huyo ambaye ana nafasi nzuri ndani ya chama tawala huku akisema serikali ina mkono mrefu, kila kitu kitakuwa wazi.
Gazeti hili linampa pole Kibanda na kumuombea kwa Mungu apone haraka - Mhariri.

HII SASA NI KALI WANANCHI

DENTI ALIYEPIGA PICHA ZA UTUPU ADAIWA KUTENGWA NA FAMILIA

Na Mwandishi Wetu
YULE denti wa chuo kimoja jijini Mwanza ambaye wiki iliyopita tuliandika habari ya picha zake za utupu kuzagaa kwenye mtandao wa BBM, Fatuma Omari amejikuta kwenye wakati mgumu kufuatia madai kuwa familia yake imemtenga.
Denti Fatuma Omari akiwa katika pozi.
Chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, mara baada ya kutoka kwa habari hiyo, baadhi ya ndugu zake walikasirika na  kutaka kujua undani wake.
“Ile stori ilipotoka ndugu wa Fatuma hawakuamini kuwa kweli kapiga picha hizo.
“Kwa bahati kuna mtu aliyekuwa na picha hizo, walipoziona, waliumia sana na baadhi wakafikia hatua ya kusema hawana radhi naye,” kilidai chanzo hicho.
Ijumaa lilimtafuta Fatuma ili kuzungumzia madai hayo bila mafanikio ila kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Saleh baada ya stori kutoka, alilipigia simu Ijumaa na kusema:
“Fatu ni mdogo wangu, nashangaa mmemuandika kuwa kapiga picha chafu wakati siyo kweli. Kama hizo picha zipo nitakuja kuziona laa sivyo tutapelekena mahakamani,” alisema Saleh.
Tumeamua kutumia picha hiyo chafu hapo chini aliyopiga Fatuma ili kuonesha uhalisia.

Jumamosi, 9 Machi 2013

TUMSAIDIENI HUYU MTOTO KAMA KWELI IMETUGUSA

           Mtoto mwenye umri wa miaka 8 nchini,anakabiliwa na uvimbe ambao ulimuanza tangu akiwa mdogo mwenye umri wa miaka mitatu..

Mzazi mlezi wa mtoto huyu akiongea na waandishi wa habari nchini,anaomba msaada wa hali na mali ili kuweza kufanikisha matibabu ya kina ya mtoto huyu nchini india..

Kama umeguswa na Hali mbaya inayomkabili mtoto huyu,Wasilisha mchango wako kupitia akaunti # 0715100784 Tigo Pesa..

Mchango wako ndiyo utakaofanikisha mtoto huyu kufanikisha matibabu yake nchini India..(Habari Picha na Amar Jamal)

CAN YOU READ THIS AND BE POLITE..?

Deadly Superstition: Albino Children Face Discrimination, Amputations And Murder In East Africa

By | March 07 2013 12:37 PM
Tanzania Teen With Albinism Photo: Reuters/Alex Wynter/IFRC A teenage Tanzanian girl with albinism sits in the female dormitory at a government-run school for the disabled in Kabanga, in the west of Tanzania near the town of Kigoma on Lake Tanganyika.

Ijumaa, 8 Machi 2013

NAPO NCHINI KENYA


Hesabu za kura 'zampa ushindi Kenyatta'

 9 Machi, 2013 - Saa 04:53 GMT
Uhuru Kenyatta
Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka raundi ya pili ya uchaguzi. Takwimu kutoka tume ya uchaguzi zinasema Kenyatta ameshinda asilimia hamsini nukta tatu za kura zote zilizopigwa.
Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu hiyo kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada yawakenya kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu na kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya uchaguzi.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila Odinga akipata 5,340,546
Kenyatta anakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.
Waandishi wa BBC wanasema iwapo Kenyatta atakabidhiwa ushindi katika raundi ya kwanza, mpinzani wake waziri Mkuu Raila Odinga atakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Tume ya uchaguzi itatangaza matokeo rasmi ya mshindi baadaye leo
Tume hiyo pia itatangaza mshindi wa uchaguzi huo na vile vile kama mshindi huyo ametimiza masharti ya kikatiba ya kutangazwa kuwa rais wa nne wa Kenya.
Kamishna Yusuf Nzibo alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume Isaack Hassan.
Vile vile mgombea huyo pia lazima awe ameshinda asilimia 25% katika nusu ya County zote 47 nchini kenya.
Awali Waziri Mkuu Raila Odinga alikuwa amewaalika waandishi wa habari nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili azungumzie maswala ya matokeo ya urais lakini baadaye mkutano huo uliakhirishwa hadi siku ya Jumamosi , baada ya tume ya uchaguzi kutoa tangazo lake la mwisho.

WATAMBUA


Muda wa mwisho wa jeshi la Ufaransa Mali.?

 7 Machi, 2013 - Saa 11:46 GMT
Jeshi la Ufaransa limekuwa likisaidia majeshi ya Afrika kupambana na wapiganaji wa Mali kwa muda sasa
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, amesema kuwa nchi yake itaanza kuondoa wanajeshi wake kutoka Mali mwezi Ujao.
Aliongeza kuwa harakati za mwisho za jeshi dhidi ya wapiganaji wa Mali zitaendelea hadi mwishoni mwa Machi kufikia Aprili.
Bwana Hollande alisema kuwa harakati hizo zilipelekea kuuawa kwa viongozi wa wapiganaji, ingawa hakuwataja majina.
Mwanajeshi mmoja wa Ufaransa aliuawa pamoja na wapiganaji 10 wakati wa makabiliano kati yao, kilomita miamoja Mashariki mwa mji wa Gao.
Bwana Hollande alisema kuwa viongozi wa wapiganaji wameangamizwa ingawa haijulikani ikiwa anazungumzia viongozi wawili waliouawa wiki jana.
Nchi ya Chad, imesema kuwa wanajeshi wake, waliokuwa wanasaidiana na wanajeshi wa Ufaransa, waliwaua makamanda wawili wakuu wa wapiganaji,Abdelhamid Abou Zeid kutoka kundi la al-Qaeda na kiongozi mkongwe wa wapiganaji wa kiisilamu Mokhtar Belmokhtar.
Wanajeshi wa Ufaransa hata hivyo bado hawajathibitisha taarifa hizo.
Takriban wanajeshi 4,000 wangali wako nchini Mali.
Wanajeshi wa Mali kwa ushirikiano na wanajeshi wengine kutoka katika nchi kadhaa za Afrika, ikiwemo wanajeshi elfu mbili kutoka Chad wamehusika na harakati hizo.
Ufaransa awali ilisema kuwa idadi ya wanajeshi itaanza kupungua kuanzia mwezi Machi ikiwa mipango yote ingekwenda kama ilivyopangwa.

JIANDAE NA..


Maonyesho ya filamu za Afrika yaanza

 09march, 2013 - Saa 16:41 GMT

Tuzo ya Stallion of Yennenga inayotolewa kwenye maonyesho ya Ouagadougou
Maonyesho ya filamu mia kadha kutoka sehemu mbali-mbali za Afrika na Wafrika walioko ng'ambo, zitaoneshwa katika tamasha kubwa ya utamaduni wa Afrika ambayo inaanza Burkina Faso Jumamosi.
Maonyesho hayo ya Panafrican Film and Television Festival ya Ouagadougou (FESPACO) yanafanywa kila baada ya miaka miwili.
Tuzo kubwa kabisa - Stallion of Yennenga - hupewa filamu ambayo inaonesha maisha halisi kabisa ya Afrika.
Filamu 20 za habari hasa kutoka Morocco, Algeria, Angola na Senegal zinagombea tuzo hiyo.
Ingawa Misri haikujiandikisha kwenye mashindano hata hivyo itaonesha filamu ya msanii wa Misri, Khaled Sayed, iitwayo "Stories from Tahrir".
Inaangalia changamoto ambazo Wamisri wanakabili wanapogombania uhuru.

JEE HAPO SASA..


Man United itawika bila RVP?

 28 Februari, 2013 - Saa 15:07 GMT
Robin Van Persie na Nyota wa Real Madrid Christiano Ronaldo
Aliyekuwa mcheza kiungo wa Manchester United Quinton Fortune, ana matumaini makubwa kuwa klabu yake ya zamani inaweza kuishinda Real Madrid hata bila kuwepo kwa nyota wake Robin van Persie.
Van Persie kwa sasa anauguza jeraha la kiuno, lakini anatarajiwa kuwa sawa wakati wa mechi ya marudiano katika uwanja wa Old Trafford, ambayo Manchester United ni sharti ishinde baada ya kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja katika mechi yao ya raundi ya kwanza.
"itakuwa pigo kubwa kwa Man United ikiwa Robin van Persie hatashinda, lakini jambo kuu ni kuwa ni suala la wachezaji wote kwa pamoja'' Fortune, aliliambia BBC.
" Naamini ni wakati wa Manchester United. Wachezaji wake kwa sasa wana hamu ya kushinda'' Alisema mchezaji huyo wa zamani.
Quinton Fortune
Van Persie amefunga jumla ya magoli 23 katika msimu wake wa kwanza na United katika ligi kuu zikiwemo tatu katika michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya.
Hata hivyo United ilipata pigo pale, Van Persie alipopata jeraha na kiuno wakati wa mechi ya na QPR siku ya Jumamosi, mechi ambayo walishinda kwa mabao mawili kwa bila.
Huenda mchezaji huyo asijumuishwe katika mechi yao ya siku ya jumamosi dhidi ya Norwich, ili kuumpa nafasi zaidi ya kupona, lakini kocha wake Sir Alex Ferguson, anatarajia kuwa atakuwa tayari kwa mechi hiyo dhidi ya mabingwa wa Uhispania.
Phil Jones, ambaye alionyesha mchezo mzuri katika safu ya ulinzi wakati wa mechi ya raundi ya kwanza, vile vile anauguza jeraha na mguu.
Fortune ameongeza kuwa mchezaji mwingine ambaye anaendelea kuimarika na ambaye anaendelea kujikita kama mchezaji wa kutegemewa katika kikosi hicho cha Manchester United ni Michael Carrick.

KWELI ULINZI UPO..?

Tisho la UN kuhusu wanajeshi wabakaji DRC

 8 Machi, 2013 - Saa 07:51 GMT
Wanawake waathiriwa wa ubakaji DRC
Umoja wa mataifa umetoa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo ichukue hatua kali za kisheria dhidi ya wanajeshi wanaoshukiwa kufanya ubakaji nchini humo.
Ujumbe wa umoja huo nchini Congo umesema kuwa utasitisha ushirika wake na vikosi viwili mahsusi vya kijeshi vilivyoshukiwa kuhusika iwapo hatua haitachukuliwa katika mwezi mmoja.
Hii imetokea huku wanawake duniani wakiadhimisha hii leo siku ya wanawake duniani.
Wanawake wengi wa eneo la maziwa makuu wameathiriwa na vita na hata hukosa huduma muhimu ya afya.

INNA LLILLAH WAINNA ILLAYHI RAAJJIUN


Hayati Hugo Chavez kuzikwa leo

 8 Machi, 2013 - Saa 08:27 GMT
Rais wa Argentina pia alifika kutoa heshima zake za mwisho kwa Chavez
Mwili wa hayati Hugo Chavez utakaushwa na kuwekwa katika makavazi ya kijeshi nchini Venezueal. Mwili wa Chavez hautazikwa kwa siku nyingine saba ili kuwaopa wananchi fursa ya kuuuona kabla ya kuzikwa.
Serikali ya Venezuela imetangaza siku saba zaidi za maombolezi kabla ya kufanyika maziko ya marehemu rais wa nchi Hito Hugo Chavez baadaye leo.
Serikali hiyo imeongeza muda wa maombolezi kufuatia kufurika zaidi watu wanaotaka kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.
Makamu wa rais , Nicolas Maduro, amesema kuwa mwili wa bwana Chavez utakaushwa na baadae kuwekwa ndani ya kaburi la vioo ambapo utakuwa ukionekana.
Amesema kuwa serikali imeamua kuchelewesha uamuzi wa mazishi yake kwasababu zaidi ya raia milioni mbili wamekuwa wakipanga mstari kwa saa nyingi kwa ajili ya kupokea jeneza la chavez linalopita.
Maafisa wanasema kuwa bwana Maduro ataapiishwa kama rais wa mpito baadaye leo na uchaguzi kufanyika baadaye.
Hugo Chavez, aliyeongoza Venezuela kwa miaka 14, alifariki baada ya kuugua Saratani kwa zaidi ya miaka miwili.
Zaidi ya viongozi 30 kutoka nchi mbali mbali wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Chavez baadaye leo akiwemo rais wa Iran,Mahmoud Ahmadinejad, rais wa Cuba Raul Castro na rais wa Belarus Alexander Lukashenko.
Rais Ahmadinejad amemsifu Chavez kama mpigania haki na kiongozi mwenye kuleta mageuzi.
Wabune wawili wa bunge la Congress la Marekani watawakilisha nchi hiyo katika mazishi haya ikikumbukwa kuwa Chavez alikuwa mkosoaji mkubwa wa Marekani.

KWA HAWA WANAFUNZI LAKINI..?

Stori: Mwandishi Wetu
MBALI na mfumo mbaya wa elimu unaolalamikiwa na wadau nchini kwamba umechangia matokeo mabaya ya kidato cha nne, lakini vitendo wanavyovifanya wanafunzi wakiwa shuleni pia vina mchango wa matokeo mabaya, Amani limechimbua.
Mitandao mbalimbali ya Bongo, imerusha picha kadhaa zikiwaonesha wanafunzi wakiwa katika vitendo vinavyoashiria ufuska, usagaji na ngono. Amani lilipata bahati ya kuzungumza na wadau, walimu na wazazi ambapo baadhi yao walikiri kuwa kuna wanafunzi wanaoendekeza vitendo vichafu wakiwa shuleni hali inayosababisha kufanya vibaya katika mitihani.
“We fi kiria, mwanafunzi wa kike anakwenda shuleni akiwa na simu yenye intaneti, anaona matukio machafu ya duniani, huyu anaweza kuzingatia masomo kweli? “Mbaya zaidi, vitendo wanavyoviona kwenye mitandao na wao huviiga kwa kuvifanya wenyewe kwa wenyewe,” alisema Bakari Mzuri, mkazi wa Magomeni, Dar es Salaam.
Ikazidi kuelezwa kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi wa kike wana uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wa kiume au watu wazima wa mitaani.
Pia imebainika kuwa wapo wanafunzi, hasa wa vyuo, wanapofunga shule badala ya kurudi kwa wazazi wao kusaidia majukumu ya
kifamilia wanakwenda kuishi na wapenzi wao sehemu nyingine huku wakidanganya makwao kwamba wametakiwa kubaki zamu.
Matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012 yanaonesha hivi:
Divisheni 0 ni 240,903 (60.1%), divisheni IV ni 103,327 (26%), divisheni III ni 15,426 (3.9%), divisheni II ni 6,433 (1.6%) na divisheni I ni 1,641 (0.49%).
Wakati huohuo, wazazi nchini wamelalamikia matumizi tofauti ya vitabu vya masomo wakisema pia yanachangia matokeo
mabaya ya mitihani.
Walitoa mfano kwa kusema kuwa, utakuta kitabu cha hesabu darasa la nne shule ya msingi ya serikali siyo kinachotumika
shule za msingi za binafsi, hali inayosababisha uelewa tofauti wa wanafunzi.

SIKIA HII WANANCHI,KWELI..?

BABA KANUMBA HANA MPANGO WA KULIONA KABURI LA MWANAYE!

Na Mwandishi Wetu
IMEBAINIKA kuwa baba wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa hana mpango wa kwenda kuliona kaburi la mwanaye lililopo Kinondoni, jijini Dar.
Baba wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa.
Taarifa zisizo na shaka, mzazi huyo amewatia wasiwasi watu wengi kwamba huenda si baba mzazi kwani tangu mwanaye afariki dunia Aprili 7, mwaka jana hajawahi kufika kulitazama kaburi achilia mbali kuhudhuria mazishi yake.
Alipopigiwa simu na kuulizwa juu ya taarifa hizo za kutofika kwenye kaburi la mwanaye, mzazi huyo alisema asiulizwe ishu hiyo.
“Sitaki kuzungumzia ishu hiyo. Una swali lingine?” aliuliza na kukata simu.

JEE,?WAJUA KUHUSU

ODAMA, MUSA BANZI KIMENUKA

Stori: Hamida Hassan
PRODYUZA mkongwe Bongo, Musa Banzi amegombana na staa wa sinema za Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ kwa kumtosa kuweka picha yake kwenye kalenda aliyoiandaa.
Kwa mujibu…

NAMNA HII KWELI..?

MISS KINONDONI APIGA PICHA ZA UTUPU

Jee wajua kuhusu gazeti la amani lina nini ndani yake..?

CHANGUDOA AMUUMBUA MCHUNGAJI,... SAJUKI AMTOKEA MTOTO WA MIAKA 5