Maonyesho ya filamu za Afrika yaanza
09march, 2013 - Saa 16:41 GMT

Maonyesho ya filamu mia kadha
kutoka sehemu mbali-mbali za Afrika na Wafrika walioko ng'ambo,
zitaoneshwa katika tamasha kubwa ya utamaduni wa Afrika ambayo inaanza
Burkina Faso Jumamosi.
Maonyesho hayo ya Panafrican Film and Television Festival ya Ouagadougou (FESPACO) yanafanywa kila baada ya miaka miwili.Filamu 20 za habari hasa kutoka Morocco, Algeria, Angola na Senegal zinagombea tuzo hiyo.
Ingawa Misri haikujiandikisha kwenye mashindano hata hivyo itaonesha filamu ya msanii wa Misri, Khaled Sayed, iitwayo "Stories from Tahrir".
Inaangalia changamoto ambazo Wamisri wanakabili wanapogombania uhuru.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni