Ijumaa, 15 Machi 2013

KWENYE

‘BIRTHDAY’ YA MTOTO WA SAJUKI,MAJONZI MATUPU

Na Imelda Mtema
‘BIRTHDAY’ ya mtoto wa aliyekuwa msanii wa filamu Bongo, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ na mjane wake, Wastara Juma, Farheen ilikuwa ni simanzi tupu, Ijumaa lina fulu data.
Katika pati hiyo iliyofanyika nyumbani anapoishi Wastara, Tabata-Bima, Dar hivi karibuni wakati mtoto huyo akitimiza mwaka mmoja, pamoja na kukamilika katika kila idara lakini kukosekana kwa baba wa mtoto (Sajuki), ndiko kulikoibua huzuni.
Habari zilieleza kuwa Sajuki alikuwa mtu muhimu kwenye pati hiyo kwani siku zote alikuwa akiisubiri siku hiyo ya kuzaliwa mtoto wake kipenzi kabla ya kukutwa na umauti Januari 2, mwaka huu.
Huku kila kona nyumbani hapo kukitawaliwa na huzuni kwa wahudhuriaji, mtoto huyo aliwaondoa watu kwenye simanzi baada ya kuonesha uchangamfu wa ajabu hadi kusababisha mama yake na wageni wengine waalikwa kuchangamka vilivyo kama vile alikuwa anatimiza zaidi ya umri wa mwaka mmoja.
Katika hali ya kushangaza, pamoja na kutulizwa lakini Farheen aliendelea kung’ang’ania kufanya kila kitu mwenyewe hasa lilipofika suala la ukataji wa keki.
Katika mahojiano na Ijumaa juu ya tukio hilo, Wastara alisema kuwa alifarijika mno kumwona mwanaye akiwa na furaha tena mchangamfu kupita kiasi kwani alimfanya asahau machungu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni