DENTI WA CHUO AUMBUKA BBM

DENTI wa chuo kimoja kilichopo jijini Mwanza (jina tunalihifadhi) aliyefahamika kwa jina la Fatma Omar amejikuta akiumbuka kwenye mtandao wa BBM baada ya picha zake chafu alizokuwa ‘akimfoadia’ mpenzi wake kuvuja.
Baada ya Ijumaa kuzinasa picha hizo na kubahatika kupata namba zake, mwandishi wetu alimpigia simu Fatma ili kujua kilicho nyuma ya pazia ya picha hizo ambapo alifunguka:
“Jamani hizo picha anayezisambaza ni mwanaume aliyekuwa mpenzi wangu anayeishi Arusha, anaitwa Amin Lema. Siku moja usiku aliniomba nimtumie nikafanya hivyo nikiamini hawezi kunifanyia mchezo mbaya.
“Juzi akaniomba nimtumie pesa kama ambavyo ilikuwa desturi yake, nikamnyima na ndipo uhusiano wetu ukavunjika. Baadaye nikasikia picha zangu za utupu zimevuja, kwa kweli sikuwa na jinsi na nilijua zitafika kwenu ‘so’ fanyeni mnavyoweza,” alisema Fatma.
Jitihada za kumpata Amini hazikuweza kuzaa matunda mpaka tunakwenda mtamboni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni