Tisho la UN kuhusu wanajeshi wabakaji DRC
8 Machi, 2013 - Saa 07:51 GMT

Wanawake waathiriwa wa ubakaji DRC
Umoja wa mataifa
umetoa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo ichukue
hatua kali za kisheria dhidi ya wanajeshi wanaoshukiwa kufanya ubakaji
nchini humo.
Ujumbe wa umoja huo nchini Congo umesema kuwa
utasitisha ushirika wake na vikosi viwili mahsusi vya kijeshi
vilivyoshukiwa kuhusika iwapo hatua haitachukuliwa katika mwezi mmoja.Hii imetokea huku wanawake duniani wakiadhimisha hii leo siku ya wanawake duniani.
Wanawake wengi wa eneo la maziwa makuu wameathiriwa na vita na hata hukosa huduma muhimu ya afya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni