ILIKUWA LAZIMA WAFELI

MBALI na mfumo mbaya wa elimu unaolalamikiwa na wadau nchini kwamba umechangia matokeo mabaya ya kidato cha nne, lakini vitendo wanavyovifanya wanafunzi wakiwa shuleni pia vina mchango wa matokeo mabaya, Amani limechimbua.

“We fi kiria, mwanafunzi wa kike anakwenda shuleni akiwa na simu yenye intaneti, anaona matukio machafu ya duniani, huyu anaweza kuzingatia masomo kweli? “Mbaya zaidi, vitendo wanavyoviona kwenye mitandao na wao huviiga kwa kuvifanya wenyewe kwa wenyewe,” alisema Bakari Mzuri, mkazi wa Magomeni, Dar es Salaam.
Ikazidi kuelezwa kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi wa kike wana uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wa kiume au watu wazima wa mitaani.
Pia imebainika kuwa wapo wanafunzi, hasa wa vyuo, wanapofunga shule badala ya kurudi kwa wazazi wao kusaidia majukumu ya
kifamilia wanakwenda kuishi na wapenzi wao sehemu nyingine huku wakidanganya makwao kwamba wametakiwa kubaki zamu.
Matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012 yanaonesha hivi:
Divisheni 0 ni 240,903 (60.1%), divisheni IV ni 103,327 (26%), divisheni III ni 15,426 (3.9%), divisheni II ni 6,433 (1.6%) na divisheni I ni 1,641 (0.49%).
Wakati huohuo, wazazi nchini wamelalamikia matumizi tofauti ya vitabu vya masomo wakisema pia yanachangia matokeo
mabaya ya mitihani.
Walitoa mfano kwa kusema kuwa, utakuta kitabu cha hesabu darasa la nne shule ya msingi ya serikali siyo kinachotumika
shule za msingi za binafsi, hali inayosababisha uelewa tofauti wa wanafunzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni